Habari za michezo

MANARA AITOA YANGA KWENYE MBIO ZA UBINGWA…AWAPA ‘MAKAVU LIVE’ MASHABIKI WAO…

admin April 25, 2022 4:00 pm


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema licha ya timu yao kuongoza Ligi mpaka sasa bado hajipi nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa.

Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 54 kwenye mechi 20 huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na 41 kwenye 19.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Manara amesema kihesabu ubingwa upo mikononi mwao lakini kiuhalisia bado wanatakiwa kupambana kukusanya pointi.

Manara amesema jambo kubwa ni kupambana na kuhakikisha wanafikisha pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile.

“Yanga bado haijawa bingwa mashabiki wanatakiwa watambue hilo, tuendelee kupambana kwa pamoja licha ya kutamba msimu ni wetu lakini pointi ndio kitu muhimu,” amesema Manara.

Yanga Aprili 30 watakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni.

NABI AIPUUZA SIMBA….AKACHA MAANDALIZI YA DABI…ARINGIA UBORA WA KIKOSI… KUELEKEA MECHI NA SIMBA..KAZE AVUNJA UKIMYA YANGA….JULIO AKUBALI YAISHE..ADAI YANGA NI BABA LAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply