Habari za michezo

A-Z JINSI YANGA NA SIMBA ZILIVYOPAPATUANA BILA KUTOBOANA JANA…YANGA YAENDELEZA UBABE….

admin May 1, 2022 2:34 am


PAMBANO la watani wa jadi kati ya Yanga ambaye alikuwa mwenyeji na Simba limemalizika kwa matokeo ya sare ya bila kufungana ikiwa ni pambano la raundi ya pili ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na ufundi mwingi lakini pia uchache wa nafasi za mabao umelalamikiwa na wadau wengi wa soka kuwa ulikuwa ni mchezo ambao timu zote ziliangalia matokeo baada ya mchezo kuliko matokeo ndani ya mchezo, kwa maana zilicheza kwa tahadhari ya kuogopa matokeo ambayo yangeweza kupatikana mwisho wa mchezo

Kutokana na matokeo hayo klabu ya Yanga inaendelea kujikita kileleni ikiwa na jumla ya alama 55 ikifuatiwa na mahasimu wao klabu ya Simba ambayo ina jumla ya alama 42 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Baada ya mchezo huu klabu ya Yanga inatarajiwa kwenda mkoani Kigoma kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Ruvushooting unaotarajiwa uchezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

HAMTUWEZI….INONGA NA MAYELE NI ZAIDI YA BALAA….AUCHO AMTIA CHAMA MFUKONI KAMA NOTI YA BUKU… RASMI…CHELSEA YAINGIA ZAMA MPYA….YAPATA MMILIKI BILIONEA MPYA…NI MMAREKANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply