Habari za michezo

MAN CITY WAIZIDI UBABE LIVERPOOL…WATETE UBINGWA WAO WA EPL KWA STAILI YA ‘KIZA KINENE’…

admin May 22, 2022 5:23 pm


MANCHESTER City wameweza kutetea taji lao la Ligi Kuu England baada ya kuweza kupindua meza mbele ya Aston Villa.

Katika dakika 45 za mwanzo Aston Villa walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0 lakini kipindi cha pili waliweza kushuhudia wakifungwa mabao 3-2 na kuifanya City kufikisha pointi 93 ndani ya Ligi Kuu England.

Liverpool wao wameshinda mabao 3-1 ugenini dhidi ya Wolves na wanaishia nafasi ya pili wakiwa na pointi 92 wote wakiwa wamecheza mechi 38.

Tukio la leo ni kama limejirudia tena kwenye Ligi Kuu England, ambapo misimu nane nyuma , Man City walitwaa ubingwa kwa staili hii ya dakika za mwisho, ambapo walikuwa wakifungana pointi na Man United.

Hii inakuwa ni muendelezo wa rekodi nzuri zinazowekwa na Man City chini ya kocha wake Mhispania Pep Guardiola, ambapo toka amekabidhiwa kikosi cha matajiri hao wa jiji la Manchester, amekosa ubingwa huo mara tatu tu.

FT: GEITA 1-1 SIMBA SC ….MPOLE AZIDI KUTAKATA…KIBU AWAOKOA NA AIBU YA KIPIGO…YANGA SASA BADO NNE TU…. TATIZO KWISHAAA…MKALI WA MABAO ATUA MSIMBAZI…KOCHA AS VITA AWAPA YANGA STRAIKA… YAIFANYIA SIMBA UMAFIA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply