Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA MAYELE KUUZWA NA YANGA…SENZO AZITAJA KAIZER CHIEF NA BERKANE…ATOA ANGALIZO HILI…

admin June 9, 2022 2:30 pm


Ofisa Mtendaji mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa amesema klabu imepokea ofa mbili kwa nyota wao, Fiston Mayele.

Amesema Kaizer Chief na Berkane zimeonyesha kumtaka nyota huyo wa kupachika mabao Yanga.

“Lakini kama klabu hatumuuzi,” amesema Senzo.

Katika hatua nyingine, Senzo ni kama amewakosha mashabiki wa Yanga baada ya kusisitiza kuwa kombe la ubingwa watalichukua palepale baada ya mechi yao kabla ya Ligi kuisha.

Yanga inahitaji ushindi kwenye mechi ijayo na Coastal ili kutangaza ubingwa.

Kama itashinda, Bodi ya Ligi imesema watakabidhiwa kombe lao siku hiyo hiyo kama watashinda.

Huku akikoleza kauli ya Bodi, Senzo alisisitiza ubingwa ni pale pale, akimaanisha kwenye mechi ijayo, jambo ambalo lilisababisha watu kuangua kicheko.

MAMBO YAZIDI KUMWENDEA KOMBO MWAKINYO….KAPOROMOKA KWA NAFASI 16 VIWANGO VYA UBORA DUNIANI… TARAJIA KATI YA MAJEMBE HAYA 13 , WATANO NI UHAKIKA WATAKIPIGA SIMBA MSIMU UJAO…MO DEWJI ARUDI RASMI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply