Geita Gold FC

KUHUSU ISHU YA MPOLE KUTUA SIMBA…GEITA GOLD WAVUNJA UKIMYA…WAIBUKA NA TAMKO HILI…

admin July 15, 2022 2:57 am


Klabu ya Geita Gold yenye maskani yake Mkoani Geita, imesema hatma ya mshambuliaji wao George Mpole ni kuendelea kusalia katika klabu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukutana na wandishi wa habari Afisa Habari na Mawasiliano wa Geita Gold, Samwel Dida amesema mpaka sasa hawajapata Ofa yoyote kutoka moja ya vilabu vikubwa hapa nchini huku akisema Mchezaji huyo yuko huru kuzungumza na klabu yoyote.

Mpole ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika akiwa na mabao 17. Amekuwa akihusishwa kisajiliwa na vilabu vikubwa nchini ikiwemo Simba na Yanga.

Katika hatua nyingine Dida amesema kwa sasa klabu hiyo itaachana na wachezaji sita huku wengine wakipelekwa kwa Mkopo katika vilabu vya hapa nyumbani na kubainisha kufanya usajili wa wachezaji wawili kutoka Cameroon pamoja na Congo.

ZORAN : NATAKA KUFIKA MBALI NA SIMBA….YANGA NAIJUA KIDOGO SANA…NINGEPEWA MIAKA MINNE INGEKUWA POA SANA… MAYELE APANGA KUITUMIA SIMBA SC KUJITAMBULISHA …”SITATETEMA TENA”….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply