Habari za michezo

KUELEKEA MSIMU UJAO….KMC FC NAO WAONA ISIWE TABU…WAIBUKA NA KUSAJILI KIFAA HIKI HATARI KUTOKA AZAM FC…

admin July 24, 2022 4:38 pm

Kiungo Mshambuliaji wa Azam FC, Awesu Awesu amejiunga na klabu ya KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Azam Awesu sasa amesajiliwa rasmi na klabu ya KMC ambayo aliitumikia kwa mkopo na kufanikiwa kuonesha kiwango kikubwa kwenye kikosi hicho.

Awesu ambaye alisajiliwa na klabu ya Azam akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, wakati akiwa kwenye kikosi cha Azam FC kiungo huyo hakufanikiwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa chini ya kocha Lwandamina na kupelekwa kwa mkopo kwenye kikosi cha KMC.

Akizungumzia usajili huo, Awesu amesema kuwa;

“Mkataba wangu na Azam umemalizika lakini tayari nimesaini mkataba wa mwaka mmoja na KMC.

“Ni changamoto mpya kwangu lakini hiyo hainipi shida kwani nimecheza kwa msimu uliopita hivyo nitaendelea kupambana.”

SHAFII DAUDA AIBUKA NA HAYA SAKATA LA MANARA KUFUNGIWA NA TFF…AWASHUKIA WANAOMTETEA KISA UYANGA WAKE… MSIMU WA KWANZA WA AZIZ KI KATIKA MZIMU WA MAYELE…ASIPOANGALIA ANAWEZA KUWA KAMA SAPORNG…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply