Habari za michezo

WAKATI SIMBA WAKIPAMBANA NA MANZOKI…MAMELOD SUNDOWNS WASAJILI KIFAA CHA TIMU YA TAIFA CHILE….

admin July 27, 2022 8:00 am


Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji raia wa Chile, Marcelo Allende.

Kabla ya kutua Mamelodi, Marcelo (23) alitokea klabu ya Montevideo City Torque inayoshiriki ligi Kuu ya Uruguay.

Nyota huyo alikuwa nahodha kwenye timu ya taifa ya Chile (U-17) kwenye mashidano ya Kombe la Dunia kwa vijana 2015.

Katika misimu miwili aliyocheza kwenye klabu ya Montevideo kuanzia 2020 hadi 2022 alicheza jumla ya michezo 87 akifunga mabao 16 na kusaidia (Assisti) 23.

Klabu yake tayari imeshamuaga kiungo huyo mshambuliaji na imemtakia kila la kheri kwenye safari yake ya soka.

KUHUSU ISHU YA MAYELE KUTAKIWA KAIZER CHIEF….NABI AFUNGUKA A-Z DILI ILIVYO NA UKWELI WA MAMBO… ISHU YA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…NGOMA BADO NGUMU….VIPERS WAKOMAA WALIPWE MIL 450…SIMBA WACHOMOA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply