Habari za michezo

UKWELI KUHUSU OKWA KUTUA BONGO BADALA YA MISRI WALIKO SIMBA UKO HIVI….MAMBO YAPELEKWA KIMYA KIMYA …

admin August 3, 2022 7:03 am


Kiungo mshambuliaji raia wa Nigeria, Nelson Esor Okwa tayari amewasili Tanzania usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Simba Sc.

Okwa ambaye alikuwa akikipiga katika Klabu ya Rivers United amewasili kwa ndege ya Shirika la Ethiopian Airlines na kufichwa kwenye moja ya hoteli iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Okwa baada ya kuwasili asubuhi ya leo Jumatano atakamilisha taratibu zake za kujiunga na Simba na huenda muda wowote akatambulishwa kama mchezaji mpya wa kikosi hicho.

Baada ya Okwa, Simba pia inatarajia kumsajili mshambuliaji mwingine wa kigeni ambapo Cesar Manzoki wa Vipers ya Uganda anatajwa.

Ikumbukwe wakati wa uzinduzi wa wiki ya Simba CEO, Barbara Gonzalez alisema hawajakamilisha kutangaza wachezaji waliowasajili.

PAMOJA NA KUAMUA KURUDI TZ…NABI ATOA KILIO CHAKE KWA TFF…AFUNGUKA JUU YA KINACHOMTESA NA YANGA YAKE… RASMI….AL AHLY WAMFUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA LUIS MIQUISSONE…WATANGAZA KUMPIGA BEI….SIMBA MPOOO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply