Habari za Yanga
Habari za michezo

ISHU YA NKANE YANGA SC…HATMA YAKE YAWEKA WAZI…

admin December 24, 2022 8:18 pm

Daktari Mkuu wa timu ya Yanga, Youssef Mohamed amesema afya ya mshambuliaji Denis Nkane inaendelea vizuri na atashiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza Januari mosi, 2023 Visiwani Zanzibar.

Youssef amesema mbali na kumpa matibabu pia mchezaji huyo ameanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kuweka mwili sawa.

“Nkane anaendelea vizuri baada ya kumfanyia vipimo na kubaini maumivu aliyoyapata hayakuwa makubwa sana, tulichofanya ni kumwanzishia tiba mapema kwa sasa anaendelea vizuri na atakuwepo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi,” amesema Mohamed.

Nkane aliumia mgongo na paja la mguu wa kulia baada ya kugongana na mchezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 Novemba 20 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Alishindwa kuendelea na mchezo huo na kutolewa uwanjani kwa machela na kuilazimu timu yake kucheza pungufu kwa dakika 10.

HAWA HAPA MASTAA 5 WA SIMBA SC WALIOKALIA KUTI KAVU…TARAJIA LOLOTE… YANGA WAMGOMEA FEI TOTO…AZAM WAMFUATA MAMA YAKE…INONGA ANAFUATA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply