Mbwana Samatta
Habari za michezo

SAMATTA MAJI YA SHINGO UBELIGIJI… AKALIA KUTI KAVU KRC GENK….

admin January 4, 2023 3:22 pm

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye yupo KRC Genk kwa mkopo anaweza kurejea muda wowote kwenye klabu yake ya Fenerbahce.

Samatta ambaye alijiunga na KRC Genk kwa mkopo wenye kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja, amekuwa akikumbana na changamoto ya namba kwenye kikosi hicho ambacho hii ni awamu yake ya pili kukichezea.

Kitendo cha kutopata nafasi mbele ya Paul Onuachu, kimetafsiriwa na mtaalamu wa usajili nchini humo, Ekrem Konur kuwa kile kipengele chake kwenye mkataba wake wa mkopo kinaweza kisitekelezwe na badala yake anaweza kurudishwa Uturuki.

Samatta mwenye miaka 30 anamkataba na Fenerbahce hadi Juni 2024, kabla ya kuamua kurejea Ubelgiji mezani mwake alikuwa pia na ofa za Uarabuni lakini aliona kuwa bado anaweza kuendelea kucheza soka la ushindani.

KIBADENI ASHINDWA KUJIZUIA KOCHA MZUNGU KUPEWA SIMBA SC..AMTAJA MGUNDA… KIMYA KIMYA…TAMBWE ATUPIWA VIRAGO SINGIDA BIG STARS…ISHU IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply