Ajibu akiwa Singida Big Stars
Azam FC

SIKU KADHAA BAADA YA KUTUA SINGIDA BIG STARS….AJIBU ATUPA ‘JIWE LA GIZANI’ AZAM FC…

admin January 5, 2023 6:53 am

Baada ya kuondoka Azam FC, Kiungo Mshambuliaji Ibrahim Ajib kwa mara ya kwanza amefungua kinywa chake na kueleza matarajio aliojiwekea, katika sehemu ya msimu wa 2023.

Mwanzoni mwaka jana Azam FC ilithibitisha kuachana na Kiungo huyo wa zamani wa klabu za Simba SC na Young Africans zote za Dar es salaam, na kumtakia kila la kheri katika makazi yake mapya kisoka.

Ajibu amesema kwa sasa anaendelea kujiandaa vizuri huku akimuomba Mwenyezi Mungu amjaalie afya njema, ili kufanikisha mpango aliojiwekea, baada ya kuondoka Azam FC.

“Namuomba Mungu anipe afya njema nataka kwenda kuonyesha mfano, siyo kama nilishindwa kucheza Azam  kwa ajili ubora, binafsi sipendi kuongea bali nitakwenda kuonyesha vitendo,”amesema Ajibu.

Kiungo huyo ambae mwaka jana ametambulishwa katika klabu ya Singida Big star kwa mkabata wa miaka miwili, atakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa kwenye kikosi hicho baada ya beki wa kushoto, Nickson Kibabage aliyesajiliwa kutokea Mtibwa Sugar.

KIPA AFICHUA JINSI AZIZ KI ANAVYOBEBWA YANGA SC…AANIKA UZEMBE ULIPO… TP MAZEMBE WAMNYIMA RAHA NABI….AFUNGUKA A-Z JINSI WANAVYOMKONDESHA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply