Habari za Yanga
Habari za michezo

PAMOJA NA KUTUA YANGA KWA MBWEMBWE ZOTE…MUSONDA AITAMANI SIMBA….AFUNGUKA ANAVYOINGOJEA…

admin January 20, 2023 6:18 am

Baada ya kuanza kuitumikia Yanga, straika mpya wa timu hiyo, Mzambia, Kennedy Musonda, ameweka wazi kuwa anajua miongoni mwa michezo mikubwa hapa nchini ni Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba na kuweka wazi kuwa ana shauku kubwa ya kuwafurahisha Yanga hususani katika mchezo huo.

Musonda ni miongoni mwa mastaa watatu wapya ambao wamesajiliwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kupitia dirisha dogo la usajili, huku akikamilisha usajili wake na kutangazwa rasmi usiku wa Ijumaa iliyopita akijiunga kutokea ndani ya kikosi cha Klabu ya Power Dynamos ya Zambia.

Staa huyo aliichezea wananchi mchezo wake wa kwanza Jumatatu wiki hii dhidi ya Ihefu, ambapo alitumika kwa dakika 27 wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumzia mchezo wake wa kwanza ndani ya Yanga, Musonda alisema: “Nashukuru kwa kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza mchezo wangu wa kwanza ndani ya Yanga, kocha kwa kuniamini licha ya kwamba nilikosa sehemu kubwa ya maandalizi ya mchezo.

“Nilikuwa na nyakati nyingi nzuri nikiwa Zambia na kupata nafasi ya kucheza michezo mingi hususani ile mikubwa ya dabi, najua hapa Tanzania kuna dabi kubwa ya Yanga na Simba ambayo ni miongoni mwa dabi bora za Afrika, nina shauku kubwa ya kucheza mchezo huo na kuwafurahisha mashabiki.”

ISHU YA CHAMA NA KOCHA KAZI IPO…MBRAZILI ATOA MSIMAMO MKALI…JAMBO LA MORRISON YANGA LIKO HIVI… KISA YANGA…BEKI LA CHAN LAKIMBIA MASHINDANO…AFUNGUKA UNDUGU WAKE NA SAIDO WA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply