Habari za Yanga
Habari za michezo

A-Z JINSI MSHERY ALIVYOPIGWA KISU TUNISIA….YANGA WAMEHUSIKA KWA KILA KITU…

admin February 10, 2023 3:42 pm

Golikipa wa Timu ya Yanga, Aboutwaleb Mshery amefanyiwa operesheni leo mjini Sousse hapa Tunisia.

Taarifa ya daktari wa Yanga imesema operesheni hiyo imefanyika salama na Mshery anatarajia kurejea Tunis, siku ya Jumamosi kwenye kambi ya timu.

Mshery yupo nje kutokana na jeraha la goti, lakini mabosi wa klabu hiyo waliamua kumpeleka Tunisia ili kufanyiwa upasuaji na kuruhusu areje mapema uwanjani.

Mshery aliumia goti hali iliyowafanya mabosi wa Yanga kwenye dirisha dogo la usajili kumrejesha kwa mkopo Metacha Mnata kutoka Singida Big Stars ili kuziba nafasi .

Mshery amepelekwa katika hospitali aliyofanyiwa upasuaji Yacouba Songne na Kibwana Shomary ambao walirejea mapema uwanjani na Daktari wa timu hiyo.

Yanga iliondoka nchini Jumanne kwa ajili ya kuwahi mchezo wa kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia utakaochezwa Februari 12 kisha ikirejea nchini itakuwa na mchezo dhidi ya TP Mazembe na baadae kuifuata Real Bamako ya Mali.

Kipa huyo alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Yanga baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar.

KWA MZUKA MWINGI WA USHINDI NA MTONYO WA UHAKIKA…MERIDIANBET IMESOGEA ZAIDI KINONDONI.. UTAFURUKUTA WEEE…LAKINI ZIKIFIKA DK HIZI…SAKHO LAZIMA AKUTUNGUE AISEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply