KOCHA SINGIDA BS AITELEKEZA TIMU...KUTIMKIA MAREKANI...ISHU NZIMA IKO HII A-Z
Habari za michezo

KOCHA SINGIDA BS AITELEKEZA TIMU…KUTIMKIA MAREKANI…ISHU NZIMA IKO HIVI A-Z

Marce Ben Komba April 13, 2023 2:44 pm

Kikosi cha Singida Big Stars kinarudi mazoezini leo Alhamisi kwa ajili ya kujiandaa na michezo mbalimbali lakini ndani ya siku 10 zijazo kitakuwa bila ya Kocha Mkuu Mholanzi, Hans Van Der Pluijm.

Baada ya kikosi hicho kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Liti Aprili 7, Pluijm alianza safari ya kwenda Marekani kwa ajili ya kuhudhuria ndoa ya mwanaye.

Kuondoka kwake kunafanya kikosi hicho kuwa chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Ramadhan Nswanzurimo kwani hata msaidizi wa Pluijm, Mathias Lule amefiwa na mama yake mzazi hivyo amekwenda kwao nchini Uganda kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza Pluijm alisema hakuna kitakachoharibika kutokana na kuondoka kwake kwani programu zote alizoziacha ziko kwenye mikono salama na ni matumaini yake akirudi ataendelea pale walipoishia mwanzo.

“Tuna wiki mbili bila mchezo wowote lakini sikutaka kutoa mapumziko ya siku nyingi kwa sababu nahitaji bado wachezaji wanaendelea palepale kwenye hali zao za kiushindani, hivyo mipango yetu haiwezi kuathirika na hilo,” alisema.

Mchezaji wa timu hiyo, Yusuph Kagoma alisema licha ya mapumziko mafupi waliyopewa, lakini anaendelea na programu zake mbalimbali za mazoezi ili kujiweka fiti kwa ajili ya michezo ijayo.

Baada ya Polisi Tanzania, mchezo ujao kwa Singida ni dhidi ya Yanga ambao bado haujapangiwa tarehe rasmi ya kuchezwa.

ISHU YA FEI TOTO YAPAMBA MOTO…CHAMA CHA WACHEZAJI KIMEINGILIA KATI BALEKE AMFUKUZISHA KAZI KOCHA IHEFU…NI BAADA YA KUFANYIWA UKATILI HUU MKUBWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply