Habari za michezo
WAKATI ONYANGO AKIOMBA POO …KITASA HIKI HAPA KUTUA SIMBA SC…JAMAA KAKIPIGA MPAKA USA…
admin
May 11, 2023
6:56 pm
Safu ya ulinzi ya Simba inatarajiwa kuimarishwa kwenye dirisha la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao baada ya ligi kuu 2022/23 kumalizika.
Wakati kukiwa na taarifa kuwa Joash Onyango ameomba kuachwa ili akatafute changamoto kwingine, Simba imeanza mchakato wa kumsaka mrithi wake.
Jicho la kocha Robertinho Oliveira limetua kwa Abdul Rwatubyaye mlinzi wa kati wa klab ya Rayon Sports ya Rwanda.
Rwatubyaye ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Rwanda, amewahi kufanya kazi na Robertinho wakati akiinoa Rayon msimu wa 2018/19.
Alirejea Rayon msimu uliopita baada ya kucheza soka la kulipwa nchini Marekani kwa misimu miwili.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.