Habari za Simba leo
Habari za michezo

BAADA YA OKRAHA KUTANGAZWA KUSEPA …MGUNDA AVUNJA UKIMYA SIMBA…ABAINISHA KINACHOFUATA..

admin June 6, 2023 1:42 pm

Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amefunguka kuhusu kiungo wa timu hiyo, raia wa Ghana, Augustine Okrah kumalizana na Simba na kuondoka Klabuni hapo.

Mgunda amesema kuanzia sasa Okrah sio mchezaji tena wa Simba na hawatamtumia tena kwenye ichezo iliyosalia kumalizia Ligi.

“Ukweli ni kwamba Simba tayari wameshamalizana na mchezaji Okrah, pamoja na kwamba ni majeruhi na asingeweza kucheza kwa sababu ya majeruhi yake, lakini tayari ameshamalizana na klabu na si mchezaji wa Simba tena.

“Nilitaka niliweke hili sawa ili lisije kuleta sintofahamu. Okrah na Simba wamepatana kama walivyopatana na wameelewana kwa hiyo tunamtakia kila la kheri huko aendako,” amesema Mgunda.

Okrah ambaye alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Bechem United ya Ghana na kuonyesha uwezo mkubwa lakini baadaye aliporomoka kiwango kutokana na majeruhi na sasa ameshapewa mkono wa kwaheri.

SImba itakuwa dimbani leo Jumanne, Juni 6, 2023 kucheza na Polisi Tanzania katika Dimba la Chamazi Dar.

RASMI…AL AHLY WAILAINISHIA SIMBA KWA MIQUISSONE…MABOSI MSIMBAZI WAPAGAWA NA MSHAHARA WAKE… DILI LA MBADALA WA MANULA SIMBA LAFIKIA HATUA HII…NI JAMBO LA MUDA TU MAMBO KUWA WAZI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply