Habari za michezo

YANGA KUTUMA UJUMBE AFRIKA NZIMA JUMAPILI HII, ALLY KAMWE ATAMBA

Staff Desk August 18, 2023 2:49 pm

Ofisa Habari wa Klabu ya Young Africans Sports, Alikamwe amesema kuwa watakachokwenda kukifanya dhidi ya wapinzani wao ASAS FC siku ya Jumapili zitakuwa ni salamu tosha kwa Afrika na kuitambua timu hiyo.

“Tunachokwenda kukifanya Jumapili dhidi ya ASAS FC inatakiwa Afrika ijue kuwa sisi Yanga SC ndio mabingwa wa Tanzania,” amesema Ally Kamwe.

Kamwe amewataka mashabiki wa soka, wapenzi na wanachama kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwenda kutoa sapoti yao kwa Wananchi watakapokuwa wakiipeperusha bendera ya Taifa pale Azam Complex Chamazi

”Mashabiki twendeni tukaujaze uwanja lakini pia kikosi chetu kinakwenda kuwakumbusha watu kuwa sisi ndio mabingwa watetezi na hivi ndivyo tunavyotoa salamu zetu,” amesema Kamwe.

Young Africans Sports watatupa karata yao ya kwanza kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya ASAS ya Djibout siku ya Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex Chmazi.

WEEKEND INAKUJA NA MAOKOTO NAYO YANAZIDI KUONGEZEKA…WEKA MKEKA WAKO HAPA.. MCHAMBUZI:- CHE MALONE SIO BEKI WA KUMTEGEMEA ….ANAMAKOSA MENGI MNOO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply