Habari za Yanga leo
Habari za michezo

HIZI HAPA SABABU TATU ‘KONKI’ KWA NINI YANGA ‘ITAWAFUMUA’ EL MERREIKH NDANI NNJE…

admin September 5, 2023 8:01 pm

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Young Africans wakiwa kwenye maandalizi ya kuwakabili Waarabu wa Sudan, zimetajwa sababu tatu zitakazowapa ushindi mbele ya El Merreikh.

Ni Kocha Mkuu wa El Merreikh ya Sudan Osama Nabieh ameweka wazi sababu hizo kwa kubainisha kuwa ana mtihani mzito mbele ya Young Africans kutokana na ubora wa kikosi cha Wananchi.

El Merreikh wanatarajiwa kukutana na Young Africans katika mchezo wa kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Septemba 16 katika Uwanja wa Pele nchini Rwanda.

Akizungumza kuelekea mchezo wao unaofuata dhidi ya Young Africans kocha huyo aliitaja sababu ya kwanza kuwa: “Tunatarajia kukutana na upinzani mgumu kutoka kwa Young Africans kuwa kwenye ubora wao mkubwa ambao wamekuwa wakiuonyesha katika michuano ya kimataifa katika siku za karibuni.

“Pili wenzetu wanapata faida kubwa ya kucheza michezo ya ligi kuu ambapo inawapa uwezo mkubwa wa kujijenga zaidi na kufahamu wapi kuna mapungufu na wapi kunatakiwa kufanyiwa maboresho.

Sababu ya tatu kocha huyo alibainisha kuwa: “Malengo yetu ni kuona tunafika makundi kama msimu uliopita, sisi tunayo changamoto ya kukosa mechi nyingi lakini naamini tunayo nafasi nzuri ya kufanya vyema dhidi yao na kutimiza malengo yetu,” amesema Nabieh.

SIRI ZA AZIZI KI ZAANIKWA WAZI….MAMA YAKE AFUNGUKA A-Z JINSI SIMBA WALIVYOMPAPATIKIA… BAADA YA SIMBA KUPANGWA NA AL AHLY….MIQUISSONE KAGUNA WEE KISHA AKASEMA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply