Habari za michezo

GAMONDI AWAPA ANGALIZO HILI MASTAA YANGA

Staff Desk October 11, 2023 11:57 am

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa baada ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wana kazi kubwa ya kufanya.Tayari Yanga wameshatambua kundi ambalo watakuwa kupambania pointi likiwa ni pamoja na Al Ahly ya Misri kwenye kundi hilo.

Yanga ilikuvunja rekodi ya kufuzu hatua hiyo baada ya miaka 25 kufuatia ushindi dhidi Al Merrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0 ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Rwanda, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ule wa nyumbani walishinda kwa bao 1-0.

Gamondi amesema kuwa amefurahishwa na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wao na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi lakini amewapa angalizo la kuhakikisha wanajipanga mapema kuweza kufanya makubwa kwenye hatua hiyo.

“Sasa ni muda wa kuangalia mechi zilizopo mbele yetu, tunafanya maandalizi hatua kwa hatua mechi kwa mechi, kabla ya kufikiria hatua inayofuata ya michuano ya kimataifa.

“Najua ukubwa na ugumu wa makundi ya Ligi ya mabingwa kwa sababu zinashiriki timu bora sasa lazima kila mchezaji anatambua nini ambacho tunahitaji kufanya ili tuweze kufanya vizuri kwa sababu hatuwezi kubweteka kwa kuwa tayari tumeshafika katika hatua hii maana nguvu na mikakati inatakiwa kuanzia sasa kwenda mbele,” amesema Gamondi.

SIMBA WAOMBE MASTAA WAO WASIITWE MASTAA HAWA YANGA WAITWA TIMU ZA TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply