Habari za Yanga SC
Habari za michezo

ISHU YA MKUDE KUSIMAMISHWA YANGA UKWELI HUU HAPA….KARUDISHWA KUNDINI LAKINI MHHH…

admin October 12, 2023 3:41 pm

Nyota watatu wa Yanga wamerejea kikosini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuivaa Azam FC, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Oktoba 25.

Metacha Mnata, Farid Mussa na Jonas Mkude hawakuhusika kwenye mechi tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo matatizo ya kifamilia na utovu wa nidhamu, lakini sasa wameitwa kambini kujiandaa na mechi zijazo.

Metacha na Mkude walidaiwa kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu, huku Farid akiwa na ruhusa maalumu na kukosa mechi ya marudiano dhidi ya Al Merreikh, Ihefu na Geita Gold.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa atatumia kipindi hiki cha mapumziko kuboresha kikosi chake na kuleta usawa.

“Ni muda wa mapumziko, baadhi ya wachezaji wetu wamekwenda kujiunga na timu zao za Taifa. Tutaendelea na mazoezi na hawa waliopo na lengo ni kuboresha na kuweka usawa wa kikosi chetu,” alisema Gamondi aliyeifikisha Yanga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 25 ikisota bila kufika hatua hiyo.

YANGA HII YA GAMONDI NI ZAIDI YA BALAA NA NUSU…MAAJABU YAKE YAWATESA SIMBA USIKU NA MCHANA… MAXI AJA NA KIAPO HIKI LIGI KUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply