Habari za Simba
Habari za michezo

KUHUSU TIMU KUFANYA VIBAYA…MANGUNGU APATA WA KUMTETEA SIMBA….

admin May 29, 2024 7:22 pm

Shabiki maarufu wa Simba SC, Kay Mziwanda amewachana viongozi wa Simba SC kuwa ndio sababu kubwa ya anguko la Simba msimu huu.

Kay ametoa kauli hiyo mara baada ya Simba kucheza mechi ya mwisho ya msimu kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar dhidi ya JKT Tanzania na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0..

“Hili anguko la Simba hata tusitafute mchawi, Meze wetu Mangungu hata hahusiki, ni viongozi ambao ndio wanahusika na usajili, wametuletea wachezaji ambao hawana uwezo wa kupambana kama vile Jobe, yule ni mchezaji wa mpira au mwanariadha?,” alihoji Kay.

Kay alimaliza kwa kuwataka viongozi kujitathimini kwani kwa misimu mitatu sasa wamekuwa wakifanya makosa yaleyale hivyo wanapaswa kuiachia timu kabla mashabiki hawajachukua hatua abaya.

KUHUSU USAJILI MPYA SIMBA, AZIZI KI, FEI TOTO NA WATAKAO ACHWA ..UKWELI WOTE HUU HAPA… AHMED ALLY:-HAKUNA SABABU YA KUTAFUTA MCHAWI ….SIMBA ILIBAKI KIDOGO TU ISHUKE DARAJA..