Home Habari za Simba Leo KOCHA WA SIMBA PATRICK AUSSEMS ARUDI BONGO

KOCHA WA SIMBA PATRICK AUSSEMS ARUDI BONGO

Habari za Simba- Patrick Aussems

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Simba SC Patick Aussems kwa misimu ya 2018-2020 amerudi tena Tanzania kuendeleza maisha ya ukocha, baada ya kuachana na AFC Leoards ya nchini Kenya.

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha huyo wa zamani wa Simba ambaye alihudumu kwa mafanikio makubwa sana, katika miaka yake miwili.

Taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 7, 2024 na kusainiwa na Afisi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Jonathan Kasano imesema Aussems atakuwa kocha mkuu wa timu hiyo kuanzia msimu ujao.

Patrick Aussems, ataanza kazi rasmi Julai Mosi ambapo sasa ataendelea na majukumu ya kukijenga kikosi hicho kwenye eneo la usajili, akishirikiana na uongozi wa klabu hiyo.

Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ataanza kazi na klabu hiyo ikiwa na jina jipya ikitoka kubadilishwa kutoka iliyokuwa Ihefu ya Mbarali kabla ya kuhamishiwa Singida na kuitwa Singida Black Stars.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaonyesha kocha huyo atakuwa na wasaidizi gani na hatma ya aliyekuwa kocha wao msimu uliopita Mecky Maxime.

Singida inakuwa klabu ya pili kwa Tanzania kumpa ajira Patrick Aussems ambaye kabla ya hapo aliifundisha Simba kwa mafanikio ikibeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili na kufikisha hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kabla kuondoka na kwenda kutafuta changamoto mpya.

SOMA NA HII  FADLU AAPA KUWAMALIZA WALIBYA...MASHABIKI WAONYWA