HABARI ZA YANGA-MZIZE
Habari za michezo

WYDAD NA MZIZE MPAKA KIELEWEKE….WATUMA OFA YA ‘KUIBEBA’ NA YANGA MAZIMA….

admin September 7, 2024 8:18 am

Klabu ya Wydad Athletic imetuma ofa ya tatu kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize, imefahamika.

Matajiri hao kutoka ligi kuu ya Morocco wameongeza dau la usajili kufikia takribani Tsh 1.4B ambapo dau hilo linaweza kuongezeka hadi kufikia Tsh 2.1B kutegemea na makubaliano ya ziada.

Aidha klabu hiyo imeipa Yanga ofa ya kufanya pre-season ya msimu ujao Morocco ambapo Wydad watagharamikia kila kitu.

Kulingana na vyombo vya habari Morocco, wanaamini ofa hiyo ni kubwa na uongozi wa Yanga utamruhusu Mzize kwenda kujiunga na timu hiyo inayonolewa na Rulani Mokoena aliyewahi kuinoa Mamelodi Sundowns.

Yanga imeweka msimamo wa kutomuuza mchezaji huyo chini ya dau lisilopungua Tsh Bilioni 2.7.

KUHUSU UFADHILI WA GSM YANGA…ENG HERSI AFUNGUKA MAZITO….ATAJA FEDHA ZINAZOINGIA… HILI HAPA JIPYA KUHUSU BALEKE NA ISHU YAKE YA USAJILI WAKE YANGA….GAMONDI ATIA NGUMU….