Habari za Simba leo
Habari za michezo

CHE MALONE, CAMARA USO KWA USO NA WAARABU….ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin March 14, 2025 1:28 pm

NYOTA wawili wa Simba SC, kipa Moussa Camara na beki Che Malone Fondoh, wanatarajiwa kurejea uwanjani kwa mchezo muhimu wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri.

Wawili hao wamekosekana kwenye michezo miwili ya Simba kutokana na majeraha lakini wanaendelea na matibabu na wanatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya pambano hilo la hatua ya mtoano.

Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, wachezaji hao wamepata takribani wiki mbili za matibabu tangu walipoumia katika mechi dhidi ya Azam FC.

β€œWamepata muda wa kutosha kwa ajili ya matibabu, na sasa afya zao zinaimarika. Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji FC, hatutakuwa na mchezo mwingine, hivyo watapata muda zaidi wa kupona na kujiandaa kwa Al Masry,” amesema Ahmed Ally.

Simba SC, wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano hayo, wataanza robo fainali ugenini dhidi ya Al Masry mnamo Aprili 2, kabla ya kurudiana nyumbani Aprili 9.

PAMOJA NA KUTOONEKANA SANA….IKANGALOMBO APEWA ‘JICHO LA TATU’ YANGA 😁😁…. ISHU YA SIMBA KUGOMEA DABI INAVYOWEZA KUIPA UBINGWA YANGA KILAINI…