Habari za michezo

BENDERA KUBWA, MAONESHO YA FATAKI NYIMBO

Vardo June 6, 2026 5:24 pm

MIAMI, MAREKANI: FIFA imezindua kile ilichokieleza kuwa ni utaratibu mpya wa kipekee na wa kuvutia zaidi wa sherehe za kabla ya kuanza kwa mechi yote ya Kombe la Dunia la 2026.

Wachezaji wote waliopo katika kikosi cha timu husika watakusanyika kuzunguka duara la katikati ya uwanja wakati wa kuimbwa kwa nyimbo za taifa, huku bendera kubwa za nchi zao zikiwa zimetandazwa uwanjani nyuma yao.

Katika Kombe la Dunia zilizopita, wachezaji 11 wanaoanza mchezo walikuwa wakisimama katika mstari mmoja wakitazama upande mmoja wa majukwaa huku watoto mascots wakiwa mbele yao.

FIFA imekuwa ikitafuta njia mpya ya kuwatambulisha wachezaji ambayo itahusisha uwanja mzima na mashabiki wote waliopo.

Katika Kombe la Dunia la Klabu la 2025, kila mchezaji wa kikosi cha kwanza alitambulishwa mmoja mmoja wakati wa kuingia uwanjani. Mfumo huo haukupokelewa vizuri kwa sababu uliongeza muda wa maandalizi kabla ya mechi, na baadhi ya michezo ilianza kwa kuchelewa.

Sasa shirikisho hilo la soka duniani linasema litaunda “sherehe ya nyuzi 360”  ambayo itatoa uzoefu wa kipekee kwa watazamaji kutoka kila sehemu ya uwanja.”

Kila mchezaji aliyeteuliwa kwenye kikosi cha siku ya mechi ataambatana na mascot na kuingia uwanjani kupitia lango maalumu.

Baada ya hapo, wachezaji wote wa timu zote mbili, ambao wanaweza kufikia 52 ikiwa kila mmoja atakuwa tayari kucheza, watakusanyika katika duara la katikati ya uwanja kwa ajili ya kutangazwa kwa vikosi na kuimbwa kwa nyimbo za taifa.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alisema:”Kadri Kombe la Dunia la FIFA linavyoendelea kukua, nasi tunaendelea kubuni njia mpya za kuwafanya watu walione na kulifurahia mchezo huu.

“Wachezaji wote pamoja na waamuzi wakikabiliana katika duara la katikati ya uwanja wakati wa nyimbo za taifa kutaunda wakati wa umoja, fahari na hisia za kipekee kwa timu na kwa kila mtu anayehusika.

Kadri mashindano yatakavyoendelea, utaratibu huo utaongezewa burudani.

BILIONEA WA QATAR AIPOTEZEA MAN UNITED DAR LEOPARDS WALIAMSHA RAGA DAR