Usajili Ulaya: Napoli Yainyatia Badiashile, Reijnders Kutimkia Saudi Arabia
Klabu ya Napoli inadaiwa kuongeza dau ili kufanikisha usajili wa beki wa kati wa Chelsea, Benoit Badiashile. Mazungumzo kati ya pande zote mbili pamoja na wawakilishi wa mchezaji huyo yameripotiwa kufikia hatua za mwisho.
Chelsea ipo kwenye mpango wa kufanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya ulinzi. Beki Trevoh Chalobah tayari amejiunga na Como, huku Maxence Lacroix akitua Stamford Bridge kutokea Crystal Palace. Lacroix anatarajiwa kuungana na Levi Colwill, Tosin Adarabioyo, na Wesley Fofana kama mabeki wakuu wa kati. Kutokana na ushindani huo, Badiashile anatajwa kuwa tayari kuondoka ili kupata nafasi ya kucheza.
Tijjani Reijnders Kutimkia Al Qadsiah Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Uholanzi, Tijjani Reijnders (28), yupo mbioni kukamilisha usajili wa Pauni 61 milioni kuelekea Al Qadsiah ya Saudi Arabia. Reijnders alijiunga na Man City msimu uliopita akitokea AC Milan kwa ada ya Pauni 46 milioni.
Barcelona Yaikomalia Bayern kwa Harry Kane Barcelona inaendelea kupambana kupata saini ya mshambuliaji wa Bayern Munich na England, Harry Kane (33). Licha ya Bayern kusisitiza kuwa haitakuwa tayari kumwachia nahodha huyo msimu huu, mabingwa hao wa LaLiga wamegoma kukata tamaa.
Man City na Man Utd Zikichuana Kumsajili Ayyoub Bouaddi Klabu za Manchester City na Manchester United zimeingia kwenye vita ya usajili wa kiungo kijana wa Lille, Ayyoub Bouaddi (18). Mchezaji huyo mwenye asili ya Morocco, anayethaminishwa kwa Pauni 85 milioni, tayari ameuambia uongozi wa Lille nia yake ya kutaka kuondoka.
Bradley Barcola Akubali Kujiunga na Liverpool Winga wa PSG, Bradley Barcola (23), anadaiwa kukubali masharti ya kujiunga na Liverpool. Hata hivyo, usajili huo wenye thamani ya Pauni 130 milioni unaweza kusitishwa ikiwa PSG haitapata mbadala wake haraka. Arsenal nayo inatajwa kufuatilia hali ya mchezaji huyo.
AS Roma Yapiga Hodi kwa Gabriel Martinelli AS Roma imeanza mazungumzo ya awali na wawakilishi wa winga wa Arsenal na Brazil, Gabriel Martinelli (25). Ingawa Martinelli anatamani kubaki Emirates, milango ya kuondoka bado ipo wazi kabla ya dirisha kufungwa.
Joao Felix Afikiria Kuondoka Saudi Arabia Mshambuliaji wa Al Nassr, Joao Felix, anafikiria kurejea Ulaya baada ya msimu mzuri nchini Saudi Arabia. Hata hivyo, anaweza kukumbana na changamoto ya kupata klabu kubwa kutokana na historia yake ya kushindwa kuingia haraka kwenye mifumo ya timu mbalimbali.
Real Madrid Yaingia Vita ya Alessandro Bastoni na Martin Zubimendi Real Madrid inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni (27). Pia, miamba hiyo ya Hispania ipo kwenye mazungumzo na Arsenal kwa ajili ya kiungo Martin Zubimendi (25).
Joao Palhinha Aelekea Aston Villa Kiungo wa Bayern Munich, Joao Palhinha (31), yupo tayari kujiunga na Aston Villa kwa mkopo. Palhinha, ambaye alicheza Spurs msimu uliopita, anawaniwa pia na Newcastle United.