Vita ya Msimamo Yaikutanisha Utrecht Dhidi ya AZ Alkmaar
Uwanja wa Stadion Galgenwaard jijini Utrecht utakuwa mwenyeji wa mchezo wa kuvutia leo Jumamosi, Agosti 15, pale FC Utrecht watakapokutana na AZ Alkmaar katika raundi ya pili ya Eredivisie.
Mchezo utaanza saa 19:45 usiku, na unawakutanisha timu mbili ambazo hadi sasa zinaonyesha hali tofauti kabisa mapema katika msimu moja ikijaribu kupona haraka, na nyingine ikitafuta kuendeleza kasi.
Wenyeji FC Utrecht wana kazi ngumu mbele yao baada ya kuanza msimu kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Groningen. Zaidi ya kukosa pointi katika mchezo huo, timu sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la majeruhi linaloathiri sehemu kadhaa za kikosi, jambo litakalomlazimu kocha kufanya mabadiliko ya kimkakati ili kukabiliana na wageni wenye nguvu.
Kwa Utrecht, mechi hii siyo tu fursa ya kupata pointi tatu za kwanza, bali pia fursa ya kuonyesha kwamba changamoto za majeruhi hazitawazuia kupambana ipasavyo nyumbani.
AZ Alkmaar wanafika Utrecht wakiwa na hali tofauti kabisa wenye kujiamini baada ya kuanza msimu kwa ushindi mzuri wa mabao 2-0 dhidi ya ADO Den Haag, matokeo yaliyowapandisha hadi nafasi ya tatu ya jedwali mapema.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. In gia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kikosi cha AZ kiko karibu kikamilifu, huku mchezaji pekee aliye nje ni Jizz Hornkamp kwa sababu za kiafya. Hali hii inampa kocha wao uhuru mkubwa wa kuchagua kikosi bora zaidi kwa safari hii dhidi ya mpinzani anayehitaji ushindi wa haraka.
Historia ndefu kati ya klabu hizi mbili inaonyesha ushindani wa hali ya juu Utrecht wana rekodi ya ushindi kumi na nne, AZ wana ushindi kumi na mbili, na sare zimefikia tisa katika michezo yao ya awali.
Usawa huu wa takwimu unaonyesha kwamba historia haitoi faida kubwa kwa upande wowote, jambo linalofanya mechi ya leo kuwa ngumu kutabirika licha ya AZ kuwa juu zaidi kwa sasa kwenye msimamo.
Kwa jumla, mechi hii itakuwa kipimo cha mapema cha uwezo wa kweli wa timu zote mbili msimu huu. Iwapo Utrecht wataweza kupanga vizuri licha ya majeruhi na kutumia fursa ya kuchezea nyumbani, wanaweza kupata matokeo mazuri yatakayowarudisha kwenye nafasi nzuri ya msimamo. Hata hivyo, AZ wana kila sababu ya kuamini wanaweza kuendeleza msimamo wao mzuri iwapo watadumisha nidhamu ile ile waliyoonyesha dhidi ya ADO Den Haag.