wachezaji wapya Simba SC
Simba SC

Wachezaji Wapya Simba SC Wabadili Kila Kitu – Ahmed Ally

Vardo October 16, 2026 9:14 am

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amefichua siri ya mafanikio ya kikosi hicho, akieleza kuwa usajili wa wachezaji wapya umeongeza ubora na ushindani mkubwa ndani ya timu.

Akizungumza hivi karibuni, Ahmed aliwataja nyota wapya akiwemo Elie Mpanzu, Libasse Gueye, Anicet Oura, na Rushine De Reuck kuwa ndio nguzo zilizeta mabadiliko makubwa na kuongeza tishio uwanjani.

Kulingana na Ahmed, viwango vya wachezaji hao vimewapa Wekundu wa Msimbazi nguvu mpya kwenye maeneo yote ya uwanja, akisisitiza kuwa ubora wao ni wa kipekee katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

“Leo ukimwangalia mtu kama Elie Mpanzu au Libasse, katika Ligi ya Tanzania hajawahi kuwa na mchezaji wa kiwango kama cha Libasse. Ukimwangalia mtu kama Anicet au Rushine, hajawahi kuwa na mtu kama yeye katika ligi,”alisema Ahmed.

Ahmed aliongeza kuwa kuwasili kwa wachezaji haoni kumeifanya Simba kuwa timu tishio zaidi, huku lengo kuu likiwa ni kutumia ushindani huo mkubwa kutwaa mataji na kuendeleza kasi yao nzuri msimu huu.

Silaha ya Simba SC CAF: Kocha Steve Barker kuwamaliza 15 de Agosto! Mapacha wa Diddy Waingia Kwenye Tasnia ya Mitindo: Maisha Yao na Kesi ya Baba Yao