Je Nani Kuondoka na Pointi 3 Siku ya Leo?
Leo hii ni nafasi ya wakali wa ligi mbalimbali kuchuana vikali kuwania ushindi wa pointi tatu muhimu kwenye ligi. Je nani kuondoka na kifua mbele?
Kule LALIGA pia kuna mechi ambapo Getafe ataumana dhidi ya Rayo Vallecano ambapo huu ni mchezo wa ushindani mkubwa zaidi huku kila timu ikihitaji kupata ushindi mnono siku ya leo.
Getafe inaweza kutegemea faida ya kucheza nyumbani, kucheza kwa ukabaji mkali na kutumia mipira ya juu pamoja na mipira iliyokufa kutafuta mabao. Hata hivyo, itahitaji umakini mkubwa ili kuepuka kupoteza mipira katika maeneo hatari.
Rayo Vallecano inaweza kujaribu kutumia kasi ya washambuliaji wake, kushambulia kupitia pembeni na kutumia nafasi zitakazopatikana wakati Getafe inapopanda mbele. Changamoto yake itakuwa kuvunja ulinzi wa Getafe na kuhimili presha ya wenyeji.
Mara ya mwisho kukutana kati yao mgeni aliondoka na ushindi hivyo hii ni mechi ya kisasi kwa mwenyeji. Je beti yako unaiweka kwa nani siku ya leo?.
Mechi hizi unazipata kule Meridianbet, lakini pia unaweza ukaangalia msimamo ya ligi mbalimbali.
Pia kule Italia SERIE A itaendelea huku mechi za kubashiri zikiwa zinakungoja wewe pekee, ni Parma dhidi ya Torino ambapo tofauti yao hadi sasa ni 3 ambapo mwenyeji yupo nafasi ya 18 na mgeni wake yupo nafasi ya 12.
EPL kitawaka haswa ambapo Tottenham atamleta kwake Conventry ambao wamepanda daraja msimu huu wakiwa wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi zao 6 hadi sasa, huku Spurs wao wakiwa nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi.
Vijana wa De Zerbi wanahitaji kupata ushindi wao wa kwanza kwenye mechi hii ya leo wakiwa nyumbani kwao kwani mpaka sasa kwenye mechi zao 6 walizocheza wamepata pointi 3 pekee kitu ambacho wanatakiwa kubadilika haraka sana.
Coventry wametoka kupata ushindi wao wa kwanza EPL tena kwa kishindo kabisa chini ya Frank Lampard kwahiyo huu utakuwa ni mchezo ambao sio rahisi kwa timu zote mbili, kwani kila timu inajitafuta na inataka kupata ushindi haraka sana.