Ligi Kuu Zanzibar: Fufuni Yapitia Mazito, Yajikuta Mkiani mwa Msimamo
TIMU ya Fufuni FC inayoonekana kupitia wakati mgumu katika Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) msimu huu wa 2026-2027, bado inatafuta ushindi wake wa kwanza baada ya kucheza dakika 720 sawa na mechi nane bila kuonja ladha ya ushindi.
Hali hii inatofautiana sana na msimu uliopita wa 2025-2026, ambapo Fufuni ilikuwa moja ya timu zilizofanya vizuri na kumaliza ligi katika nafasi ya sita kwa ushindani mkubwa. Hata hivyo, msimu huu mambo yamegeuka baada ya timu hiyo kukusanya pointi mbili pekee kati ya mechi nane ilizocheza, ikipoteza sita na kutoka sare mbili.
Katika michezo hiyo, Fufuni imefunga mabao matatu huku safu yake ya ulinzi ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 12, jambo linaloifanya kuwa timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi hadi sasa, ikifuatiwa na Black Sailors iliyofungwa mabao 11.
Matokeo ya mechi ilizofungwa ni pamoja na:
-
Chipukizi (1-0)
-
Wembe (1-0)
-
Polisi (2-1)
-
KVZ (3-0)
-
Uhamiaji (2-1)
-
Muembe Makumbi (1-0)
Sare zake mbili pekee zilipatikana dhidi ya Raskazone (bila kufungana) na Black Sailors (mabao 2-2). Mwenendo huu unaiacha Fufuni katika wakati mgumu wa kujinasua kutoka mkiani mwa msimamo na kuwataka viongozi na benchi la ufundi kufanya Mabadiliko ya haraka kabla ya mambo kuwa magumu zaidi.