Abdul Razaq Hamza kurejea Simba
Simba SC

Ahmed Ally Atamba Baada ya Abdul Razaq Hamza Kurejea Simba: “Orlando Pirates Waje Tu, Jeshi Limekamilika!”

Vardo November 15, 2026 4:03 pm

Klabu ya Simba SC imepata nguvu mpya kuelekea michezo yake ijayo baada ya beki wake kisiki, Abdul Razaq Hamza, kurejea rasmi kikosini akitokea nje ya uwanja kwa muda.

Abdul Razaq Hamza kurejea Simba kumeibua shangwe kubwa Msimbazi, huku Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, akijitokeza hadharani kueleza furaha yake na kutuma salamu nzito kwa wapinzani wao, Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Ahmed Ally alimkaribisha tena beki huyo ambaye amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi, akimtaja kama “ukuta wa nyuma” wa timu hiyo.

“Furaha mitaa ya Msimbazi kushuhudia kurejea kwa beki wetu Abdul Razaq Hamza,” aliandika Ahmed Ally, akionyesha namna urejeo wa nyota huyo ulivyorejesha morali na matumaini makubwa ndani ya kikosi.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo mgumu wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya miamba ya Afrika Kusini, Orlando Pirates, msemaji huyo hakusita kuweka wazi kuwa sasa hawana hofu na timu yoyote.

“Orlando aje na yeyote aje, jeshi letu limekamilika sasa,” alisisitiza Ahmed.

Kurejea kwa Abdul Razaq Hamza kunakuja katika kipindi muhimu ambacho benchi la ufundi la Simba SC linahitaji machaguo mapana na imara katika safu ya ulinzi ili kuhimili mikikimikiki ya mashindano ya ndani na kimataifa.

King’s Sword Yafungua Milango Ya Zawadi, Ingia Kwenye Battle For The Throne