MABINGWA watetezi Simba leo wamekabidhiwa kombe la Ligi Kuu Bara na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola baada ya kumaliza mchezo wao wa mwisho uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kwenye mchezo wa leo, Mtibwa Sugar wamelazimisha suluhu ya kutofungana wakiwa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Uhuru.
Huu ni ubingwa wa 20 kwa Simba wakiwa nyuma ya wapinzani wao wa karibu Yanga ambao wamebeba ubingwa huo mara 27.
Kesho watarejea Dar na kombe hilo huku sherehe zikianzia maeneo ya Kibaha ambapo wachezaji watapanda kwenye gari la wazi wakionyesha kombe walilotwaa msimu wa mwaka 2018/19 baada ya kufikisha jumla ya pointi 93 wakiwa nafasi ya kwanza.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.