Home Uncategorized Uwanja umeharibu fainali ya shirikisho

Uwanja umeharibu fainali ya shirikisho

BAO la dakika ya 65′ la mchezo lililofungwa na mshambulizi raia wa Zambia, Obrey Chirwa limeipata taji la kwanza la kombe la FA klabu ya Azam FC baada ya kuilaza Lipuli FC goli 1-0 katika mchezo wa fainali Ilulu Stadium, Lindi jioni hii.

Kabla ya fainali hiyo ya nne mfululizo kufanyika baada ya kurejeshwa msimu wa 2015/16, hofu ya eneo la kuchezea katika uwanja wa Ilulu ilichangia wengi kuamini mchezo huo hautakuwa na mvuto.

Kama ilivyotarajiwa, licha ya wachezaji wachache kuweza kuonyesha umahiri wao- mfano kiwango cha kumiliki mpira, kupiga chenga, kupora mipira na kupiga pasi kutoka kwa mchezaji bora wa mchezo huo, mlinzi wa kushoto wa Lipuli, Paul Ngalema, lakini kiujumla fainali hiyo licha ya kuzikutanisha timu za ligi kuu Tanzania Bara, kwa kiasi kikubwa ‘ili-doda’.

Hapakuwa na mbinu za kiufundi kutoka upande wowote na hili kwa kiasi kikubwa lilichangiwa na ugumu wa eneo la kuchezea ‘pitch’ ya uwanja huo. Goli la dakika ya 25 kabla ya kumalizika kwa mchezo kutoka kwa Mzambia, Chirwa lilitokana na juhudi binafsi baada ya mchezaji huyo alipoamua kujitoa kwa dakika chache tu kati ya dakika 90′ alizokuwepo mchezo.

Azam FC ambao wamepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika msimu ujao wa Caf Champions League wanapaswa kuboresha kwa kiasi kikubwa safu yao ya mashambulizi ambayo licha ya kwamba wana mastraika kama Mzimbabwe, Donald Ngoma na Chirwa timu hiyo haina nguvu.

Lipuli wamefanikiwa kufika fainali yao ya kwanza ya ‘kikombe rasmi’ katika kipindi chote cha miaka yao isiyopungua 60, na wamefanya hivyo ikiwa ni msimu wao wa pili tu katika ligi kuu baada ya kucheza madaraja ya chini kwa miaka zaidi ya 16.


Licha ya changamoto ya uwanja lakini kikosi hicho kutoka Iringa kimeweza kuifanya fainali ‘kuwa fainali’ na walikuwa mbele kwa umiliki wa mchezo kwa muda mwingi jioni hii. Walistahili kufika hapo na pengine wamestahili kupata walichostahilli.

SOMA NA HII  ISHU YA MORRISON YAZUA SURA MPYA, AAMBIWA ASIWE MKUBWA KULIKO TIMU

Licha ya kuonekana kuizidi nguvu safu ya ushambulizi ya Azam, beki ya Lipuli iliruhusu goli lililowanyima kikombe chao cha kwanza kihistoria kutoka na uwezo wao mdogo kimbinu, Chirwa alipoaamua kutumia nguvu mara moja tu, Haruna Shamte akashindwa kiufundi.

The post Uwanja umeharibu fainali ya shirikisho appeared first on Kandanda.