Home Uncategorized EDEN HAZARD APATA KIGUGUMIZI KUTOFAUTISHA PREMIER LEAGUE NA LA LIGA

EDEN HAZARD APATA KIGUGUMIZI KUTOFAUTISHA PREMIER LEAGUE NA LA LIGA


EDEN Hazard mchezaji wa Real Madrid ambaye leo ametambulishwa rasmi baada ya kukamilisha utaratibu wa uhamisho kutoka kikosi cha Chelsea amesema kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya Premier League na La Liga.
Hazard amesema kuwa utofauti upo ila hafikirii kama kuna ligi ambayo ni bora kuliko nyingine.
“Premier League na La Liga ni vitu viwili tofauti lakini sifikirii kama kuna ligi moja ambayo ni kubwa kuliko nyingine.
“Kuhusu jezi namba 10 mimi sina tatizo na namba ya jezi ninachofikiria ni kazi tu hamna jambo jingine kwa sasa,” amesema.
SOMA NA HII  LAMINE AIPA YANGA HASARA NYINGINE