Home Uncategorized SIMBA MAMBO NI MOTO, NYOTA WANNE WAJIONDOA

SIMBA MAMBO NI MOTO, NYOTA WANNE WAJIONDOA


BAADA ya James Kotei kusepa mazima Simba na kutimkia kikosi cha Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwa kandarasi ya miaka mitatu mambo yamezidi kupamba moto Simba.

Mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Deogratius Munish ‘Dida’ ametoa mkono wa kwa heri kwa mashabiki wa Simba.

Dida alisajiliwa na Simba kwa kandarasi ya mwaka mmoja tayari mkataba wake umemalizika na sasa ni mchezaji huru ambaye amesema anahitaji kupata changamoto mpya.

“Napenda kuwashukuru mashabiki zangu, uongozi wa Simba kwa muda ambao nimewatumikia, kwa sasa nahitaji kupata changamoto mpya,” amesema Dida.

Dida anakuwa mchezaji wa nne kuaga Simba akiungana na kiungo mnyumbulifu, Haruna Niyonzima ambaye naye amesema kuwa muda ukifika atataja sehemu atakayokuwa msimu ujao, pamoja na mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye amesema ni ngumu kusema neno kwa heri.

SOMA NA HII  VAR INAWALIZA KINOMA MANCHESTER CITY, GABRIEL JESUS HAAMINI KABISA