Uncategorized

SABABU KUBWA ZA KAHATA KUMALIZANA NA SIMBA ZATAJWA

admin July 4, 2019 5:01 pm


UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa ya Francis Kahata kusajiliwa ni uwezo wake mkubwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa pamoja na timu yake ya Gormahia ya Kenya.

Kahata mwenye umri wa miaka 27 leo amemalizana na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili.

Ataungana na kiungo mwenzake Ibrahim Ajibu ambaye naye amejiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka mwili kumlisha mipira mchezaji mwenzake wa zamani Meddie Kagere ambaye naye alikuwa mchezaji wa Gormahia.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa usajili wa Kahata ni maalumu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

“Huu ni usajili wa Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya TP Mazembe, Al Ahly wakubwa wenzetu,” amesema.

YANGA YATOA TAMKO ZITO KUHUSU WACHEZAJI WAKE WANAOWASUMBUA KUSAINI KANDARASI MPYA, ISHU YA GADIEL MICHAEL YAZIDI KUSHIKA KASI, CHAMPIONI IJUMAA LINA MAJIBU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply