Home Uncategorized YANGA YATOA TAMKO ZITO KUHUSU WACHEZAJI WAKE WANAOWASUMBUA KUSAINI KANDARASI MPYA,

YANGA YATOA TAMKO ZITO KUHUSU WACHEZAJI WAKE WANAOWASUMBUA KUSAINI KANDARASI MPYA,


MSHINDO Msolla Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa klabu ya Yanga ni kubwa kuliko mchezaji hivyo hawana presha na beki Gadiel Michael ambaye mkataba wake umemalizika ndani ya Yanga.

Msolla amesema kuwa endapo beki huyo atawasumbua kusaini watamwacha aendelee na hamsini zake kama ambavyo wamefanya kwa nyota wao Ibrahim Ajibu ambaye amejiunga na timu yake ya zamani ya Simba.

“Hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu, hata mimi cheo changu hakina maana kwamba ni mkubwa kuliko timu, hivyo kama Gadiel hatakubali kusaini hatuna haja ya kumbembeleza kwa kuwa mpira ni kazi.

“Ni wajibu wa kila mchezaji kumuheshimu mwajiri wake na kufuata masharti hivyo kama ataamua kuondoka milango ipo wazi, wengi sana wamepita Yanga,” amesema.

SOMA NA HII  PLAYOFF NGOMA NI NZITO, SASA MECHI ZA MWISHO KUAMUA