Uncategorized

KUMEKUCHA. YANGA, SIMBA KUSAJILI KWA FAINI

admin July 13, 2019 9:20 am


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zinapaswa kukamilisha usajili kwa njia ya mtandao (Tanfootball Connect) kabla ya usajili kufungwa na kwa wale ambao wanashiriki michuano ya kimataifa kwa sasa lazima wapigwe faini.


Timu ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa ni pamoja na Simba, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa huku Azam FC na KMC wakishiriki michuano ya kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa mpaka sasa hakuna timu ambayo imekamilisha kiukamilifu zoezi la usajili kwa mtandao na hakutakuwa na muda wa kuongeza.

“Dirisha la usajili likifungwa hakuna cha kusubiri ama kuongeza muda kwa wale ambao wanashiriki michuano ya kimataifa kwa sasa hawawezi kukwepa kutoa faini.

“Kwa timu zinazoshoriki mashindano ya Caf usajili bila faini umefungwa Julai 10 hivyo kuanzia Julai 11 mpaka 21 faini yao ni dola 250 watakaoendela mpaka Julai 30 watatoa faini dola 500 na wachezaji hao watacheza mzunguko wa pili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Ndimbo.

SIMBA YAAHIDI KUCHUKUA MATAJI YOTE TANZANIA – VIDEO UONGOZI WA YANGA KULA SAHANI MOJA NA WAPIGAJI WA NEMBO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply