Burudani

WEMA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

Vardo June 13, 2026 9:34 am

Muktasari:

Taarifa za kujifungua kwa staa huyo zilisambaa Ijumaa, Juni 12, 2026, na kuibua furaha mitandaoni, huku mashabiki, marafiki na watu mbalimbali wakituma salamu za pongezi kwa wawili hao.

Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amejifungua mtoto wa kiume akiwa na mchumba wake ambaye ni msanii wa Bongofleva, Whozu, na kuhitimisha safari ndefu ya kusubiri iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mashabiki wake.

Taarifa za kujifungua kwa staa huyo zilisambaa Ijumaa, Juni 12, 2026, na kuibua furaha mitandaoni, huku mashabiki, marafiki na watu mbalimbali wakituma salamu za pongezi kwa wawili hao.

Kujifungua kwa Wema kumekuja baada ya miaka mingi ya changamoto na simulizi mbalimbali kuhusu safari yake ya kutafuta mtoto, jambo ambalo amewahi kulizungumzia hadharani katika mahojiano na kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa muda mrefu, Wema amekuwa akieleza hamu yake ya kuwa mama huku akikiri kuwa suala la kutopata mtoto lilikuwa miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakimuumiza zaidi maishani mwake.

Mbali na kukabiliwa na presha kutoka kwa jamii, staa huyo pia aliwahi kufichua kuwa alipitia changamoto za kiafya zilizomlazimu kusafiri hadi India kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ovari zake mwaka 2018.

Katika safari hiyo, Wema pia aliwahi kukumbana na maumivu ya kupoteza ujauzito, lakini aliendelea kuwa na matumaini kuwa siku moja angefanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuwa mama.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume sasa kunafungua ukurasa mpya katika maisha ya Wema na Whozu, huku simulizi yake ikiendelea kugusa wengi waliokuwa wakifuatilia kwa miaka mingi safari yake yenye majaribu mengi kabla ya kufikia furaha hiyo.

SOMA ZAIDI: Safari ya Wema Sepetu kutoka kuitwa tasa, kufanyiwa upasuaji India, kupoteza ujauzito hadi hatimaye kuwa mama.

PACOME HAJAISHA TUSIANGALIE NAMBA TU MECHI ZA HESHIMA LALA SALAMA CHAMPIONSHIP