Uncategorized

MCHAKAMCHAKA WA AZAM FC KIMATAIFA NI MOTO

admin July 31, 2019 10:38 am


KIKOSI cha Azam FC kinaedelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea kwenye mchezo wao kimataifa wa kombe la Shirikisho dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia.

Azam FC ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho, watamenyana na Fasil Kenema, Agosti 10 ikiwa ni mchezo wa awali kabla ya kurudiana nao uwanja wa Chamazi, Dar.

Ofisa Habari wa Azam FC, Japhary Maganga amesema kuwa mchakamchaka unaendelea ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

“Utakuwa mchezo mgumu na mkubwa kwetu hivyo tunajipanga ili kuona namna gani tunaipeperusha Bendera ya Taifa kimataifa zaidi,” amesema.

Azam FC walitwaa ubingwa huo baada ya kushinda mbele ya Lipuli FC kwa bao 1-0 lililopachikwa na Obrey Chirwa.

LUKAKU AKISEPA TU UNITED HAWA HAPA KUVAA VIATU VYAKE MUSSA MBISSE MLINDA MLANGO ALIYEKUWA NA MALENGO YA KUWA PADRI KWA SASA YUPO MWADUI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply