Uncategorized
POLISI TANZANIA YAIPIGA MKWARA MZITO AZAM FC LEO
FRANK Lukwaro, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania amesema kuwa kikosi kipo tayari kuwavaa Azam FC leo.
Polisi Tanzania iliyo chini ya Seleman Matola leo itamenyana na Azam FC uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 mchezo wa kirafiki.
Akizungumza na Saleh Jembe, Lukwaro amesema wamejipanga kufanya vizuri kutokana na morali ya wachezaji wao.
“Tupo vema na tumejipanga ni suala la muda tu kwenye mchezo wetu, tunawaheshimu wapinzani wetu ila tutapambana kupata matokeo,” amesema.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.