Uncategorized

YANGA: EVERTON WALIKAA KWA KARIOBANGI HIVYO MECHI ITAKUWA NGUMU, MASHABIKI WAJITOKEZE

admin August 1, 2019 3:33 pm


DISMAS Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa Agosti 4 haitakuwa nyepesi kwani wanacheza na timu ngumu na watatambulisha pia wachezaji.

Ten amesema:- “Uwanja wa Taifa itakuwa ni kilele cha siku ya Mwanachi ambapo tutacheza na timu kubwa na yenye uwezo mkubwa ambayo ni Kariobangi Sharks kutoka Kenya.

“Hawa ni mabingwa wa SportPesa Super Cup na hivi karibuni imewafunga Everton hivyo si klabu ya kuwabeza na utakuwa ni mchezo mzuri.

“Agosti 4 timu yetu itatambulisha wachezaji wake wote pamoja na jezi, tunawaomba wanachama wote wanunue vifaa halisi ambavyo vinatengenezwa na mzabuni aliyeshinda tenda,” amesema.

Everton ilipomenyana na Kariobangi kwenye mchezo wa kirafiki dakika 90 walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na kupelekea kupigwa penalti ambapo Kariobangi ilishinda penalti 4-3

BENETEZ KIBOKO YA GARETH BALE, CHEKI REKODI YAKE NDANI YA REAL MADRID OKWI AFUNGA KAZI, ATUA ZAKE MISRI NA KUSAINI MKATABA HADI MWAKA 2021

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply