Uncategorized

ALICHOFANYIWA MWILI JUMBA AMBAYE NI MBADALA WA MAKAMBO NDANI YA YANGA KIBOKO

admin August 4, 2019 2:37 am


DAVID Molinga ‘Mwili Jumba’ ambaye ni badala wa Heritier Makambo jana amekiona cha moto baada ya kupewa mazoezi ya nguvu na Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera.

Mazoezi hayo ya mwisho ambayo yalifanyika uwanja wa Uhuru ni maalumu kwa ajili ya mchezo wa leo utakaochezwa uwanja wa Taifa dhidi ya Kariobangi Sharks kwenye kilele cha siku ya Mwananchi.

Zahera amesema kuwa lengo la mazoezi hayo ni kuweza kumuweka fiti mchezaji huyo ili aweze kuzoea mazingira pamoja na hali ya Dar kwani hana muda mrefu na timu.

Leo Yanga itawatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na jezi mpya zitakazotumika msimu wa mwaka 2019/20 uwanja wa Taifa.

Molinga amejiunga na Yanga kwa kandarasi ya mwaka mmoja kwa mkopo akitokea AC Lega ya Congo.

KOCHA TANZANITE: TUPO TAYARI KUWAVAA ESWATINI LEO KOCHA STARS: LEO KENYA HAWATOKI, TUPO TAYARI KUPATA MATOKEO CHANYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply