Uncategorized

IWOBI MAMBO SAFI EVERTON, AIKACHA ARSENAL MAZIMA

admin August 9, 2019 5:09 am


EVERTON imethibitisha kuinasa saini ya mshambuliaji wa kikosi cha Arsenal, Alex Iwobi.

Nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Nigeria amesaini kandarasi ya miaka mitano.

Iwobi akiwa Arsenal ambayo alijiunga nayo msimu wa mwaka 2015 amecheza jumla ya michezo 149 akiwa na washika bunduki hao.

Ameanza akiwa kijana kuwa na makazi ndani ya Emirates na amefunga jumla ya mabao 15 huku akitengeneza nafasi za mabao 27.

Everton imesema:” Kwa sasa Iwobi amesaini kandarasi ya miaka mitano na tutakuwa naye mpaka mwaka 2024 Juni. 


Bosi wa Everton, Marco Silva amesema: “Alex ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye mpango wetu kwenye dirisha hili la usajili, tunaamini atafanya maajabu,”.

TOWNSHIP ROLLERS WATUA NA MAJI YAO DAR KUCHEZA NA YANGA TAIFA – VIDEO ARSENAL YAMALIZANA NA MABEKI DAKIKA ZA USIKU, MENEJA AMPA TANO LUIZ

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply