Uncategorized

HARMONIZE AZIDI KUTIBUA MAMBO WASAFI

admin August 16, 2019 9:34 am


DAR ES SALAAM: Zile tetesi za staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ kuwa anataka kusepa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), zimeendelea ‘kutibua’ mambo. 

Tetesi hizo zimeendelea kutikisa kwenye mitandao ya kijamii Bongo tangu Harmonize au Harmo alipofuta neno ‘Signed Under WCB Label’ kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Harmo ameendelea kuwaaminisha watu kuwa huenda akaondoka au ameshaondoka Wasafi hasa baada ya kuendelea kufanya mabadiliko kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Jambo lingine linalowaaminisha watu ni kitendo chake cha kuamua ‘kum-follow’ (kuwa mfuasi) msanii hasimu wa bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kwenye akaunti yake ya Instagram.

Kitendo hicho hakuwahi kukifanya kwa muda wote akiwa Wasafi hivyo kimeibua gumzo kwa kuwa amekifanya wakati huu ambapo kuna tetesi za kuondoka kwenye lebo hiyo.

Kiba na Diamond au Mondi wamekuwa mahasimu wa kimuziki kwa muda mrefu na wasanii wote wa Wasafi hawaja-follow akaunti ya Kiba isipokuwa Harmo pekee ambaye ameamua kum-follow hivi karibuni. Kitendo hicho kimetafsiriwa kama kuzidi ‘kutibua’ mambo ndani ya Wasafi na kuwa miongoni mwa ishara kuwa Harmo yupo mbioni kuiacha au si mwanafamilia wa lebo hiyo tena.

KIONGOZI SIMBA AIOMBEA SAPOTI YANGA NYOTA YANGA AMKOSESHA AMANI KIPA TOWNSHIP ROLLERS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply