Uncategorized

NGUVU YA KIKOSI CHA KMC ZINAHAMIA HUKU KWA SASA, LEO KUANZA MITIZI YA MAANA

admin August 26, 2019 8:22 am


UONGOZI wa KMC leo unaanza rasmi mazoezi ya kuiwinda Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Agosti 27 uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwary Binde amesema kuwa kikosi kinaanza mazoezi leo uwanja wa Bora kujipanga na mchezo wao wa ligi.

“Tupo sawa na wachezaji wanatambua kuwa kazi inahamia kwenye ligi, tuna imani ya kupata matokeo kwani tupo tayari,” amesema.

Mara ya mwisho walipokutana uwanja wa Uhuru, msimu uliopita, Azam na KMC zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

ZAHERA AIZUNGUMZIA MECHI YA SIMBA VS UD SONGO ‘ MIMI SIJUI’ – VIDEO UD SONGO WALIISHINDA SIMBA KWA KUTUMIA SILAHA ZA SIMBA, WAKATI WA KUNYANYUKA NA KUSONGA MBELE NI SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply