Uncategorized

MO AZUIA TENA PRESS YA HAJI MANARA SIMBA

admin August 27, 2019 8:52 am


Inaelezwa kuwa Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amezuia tena kikao alichotakiwa kukifanya Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara.

Hii itakuwa mara ya pili sasa kuahirishwa kwa mkutano huo baada ya siku kadhaa nyuma Mo kumzuia Manara asiitishe kikao ambacho alipanga pia kukifanya.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema Mo amezuia kikao hicho kilichopaswa kufanyika leo saa sita mchana.

Haijajulikana Manara alipanga kusema nini pengine tunaweza kujua siku za usoni kipi alihitaji kuzungumza.

Wakati huo, kikosi cha Simba kimeshaanza maandalizi ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es Salaam.

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMANNE YA AGOSTI 27 2018 DAR ES SALAAM CORRIDOR GROUP KUMUONA MO SALAH LIVE ANFIELD

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply