Uncategorized

STRAIKA MAN UNITED ATUA INTER MILAN

admin August 30, 2019 8:42 am


Hatimaye Alexis Sanchez ametua jijini Milan kukamilisha dili la kujiunga na Inter Milan kwa mkopo akitokea Manchester United.

Sanchez ametua jijini hapo baada ya kudumu United kwa miezi 18 akiwa hana mafanikio makubwa lakini bado akiwa na mkataba mrefu na wababe hao wa Jiji la Manchester.

Inaelezwa kuwa Sanchez ataendelea kulipwa sehemu ya mshahara wake na Man United, ambapo Inter imekubali kulipa pauni 4.5m katika pauni 21m ambazo anatakiwa kulipwa na United kwa mwaka mmoja.

Sanchez sasa ataungana na rafiki yake, Romelu Lukaku ambaye tayari ameshatua kikosini hapo na alicheza mchezo wa wiki iliyopita katika Serie A.

HABARI NJEMA!! DUDUBAYA AOKOKA, AFANYIWA MAOMBI YA KUFA MTU RUBY AFUNGUKA KUACHANA NA MZAZI MWENZAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply