Uncategorized

MBELGIJI SIMBA AIBUKA NA KALI YA SIKU, HATAKI MPIRA WA SHOO

admin September 2, 2019 9:05 pm


Patrick Aussems amewapiga biti wachezaji wa kikosi hicho kwa kuwaambia hataki kuona wakicheza mpira wa shoo badala yake anataka kuwaona wanafunga mabao ya kumwaga. Simba wiki iliyopita ilianza Ligi kwa kuwapiga JKT Tanzania mabao 3-1 Jijini Dar es Salaam.

Mbelgiji huyo amesema kuwa aliona jambo hilo katika mchezo huo ambao walistahili kushinda mabao mengi lakini kutokana na uchezaji wa shoo na utoto ndani wakashindwa.

“Tulikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda mabao matano kwenye mechi yetu na JKT Lakini tulishindwa kwa sababu wachezaji walicheza kitoto.

 “Walikosa nafasi ya kufunga mabao hayo ya wazi, kwangu mimi sikubaliani na hali hiyo na tunatakiwa kubadilika na kuhakikisha kwamba tunafunga mabao mengi katika kila nafasi ambayo tunaitengeneza katika mechi zetu,” alisema Aussems amefeli mtihani wa kwanza kimataifa.

LIGI KUU BARA YAANZA NA REKODI BAB KUBWA ZAHERA ATUMIA DAKIKA 90 KUTENGENEZA MABAO YA BALINYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply