Uncategorized

BREAKING; LICHA YA MSUVA KUIBEBA , BOSI WA STARS ASHIKILIWA NA POLISI BURUNDI

admin September 4, 2019 5:03 pm


JESHI la Polisi la Burundi, linamshikilia msimamizi wa masuala ya mechi wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Danny Msangi.

Imeelezwa, Msangi na mwandishi mmoja wa habari kutoka Azam TV walishambuliwa na askari hao wakiwemo wanajeshi baada ya kuona wakizuia raia mmoja wa Burundi aliyetaka kupulizia dawa kwenye vyumba vya wachezaji.


 “Msangi bado yuko ndani na wameshambuliwa sana kwa ngumi na mateke.

 ” Walikuwa na Oscar wa EFM, lakini yeye aliachiwa baadaye,” kilieleza chanzo.

 Stars leo imeibania Burundi kwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza kuwania kucheza Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar na bao pekee la Stars lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 85.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba nane uwanja wa Taifa pia kwenye mchezo wa leo Stars hawakuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo muda wa mapumziko.

MSUVA AIPA AHUENI STARS BURUNDI, MECHI YAMALIZIKA 1-1 KELVIN YONDANI ATAJWA ZESCO UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply